Bayern munich wamsajili rasmi sandro

Club ya bayern munich imethibitisha kumsajili mshambuliaji wa hoffeheim sandro wegner kwa ada ya €13m.

Sandro ni zao la kituo cha kukuzia vipaji cha bayern munich (munich football academy). Aliondoka klabuni hapo mwaka 2008.

Amepitia vilabu vingi sana ikiwemo wender bremen, darmstadit, hertha berlin  , haffeheim na sasa amerudi nyumbani.

Sandro amesaini mkhataba wa miaka miwili na nusu wa kuitumikia bayern na ataanza kazi january. Lakini pia amekabithiwa jezi namba mbili.

Mukurugenzi wa bayern munich hassan salihamidzic amesema

   "tumeongeza staa mwingine wa kijerumani, kwa sandro tunaamini anakiwango sasa cha kuitumikia bayern munich"

 

 

 

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA LEO ALHAMISI

 

Swansea inajaribu kumrai mkufunzi wa zamani wa Man United Louis van Gaal kuwa meneja wake mpya baada ya kumfuta kazi Paul Clement. (Daily Mirror)


Mkufunzi wa zamani wa Stoke, West Brom na Crystal Palace Tony Pulis ni miongoni mwa wakufunzi wanaotarajiwa kumrithi Clement. (Daily Star)


Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 29, anakaribia kuhamia Paris St-Germain baada ya ajenti wake kuelekea katika mji mkuu wa Ufaransa kwa mazungumzo(Canal Plus - via Metro)


PSG itajaribu kumsajili Sanchez kwa dau la £25m ijapokuwa Manchester City bado wanamtaka mchezaji huyo wa Chile baada ya kushindwa kumpata mchezaji huyo kwa dau la £60m katika dirisha la uhamisho lililiopita. (Express)
Sanchez atasalia Arsenal mwisho wa msimu na baadaye ajiunge na Manchester City katika uhamisho wa bure , mpango ambao utampatia kipato cha £400,000 kwa wiki. (Daily Mirror)


Barcelona iko tayari kulipa £132m ili kumsajili kiungo wa kati wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Sport - via Daily mirror)


Atletico Madrid inasema kuwa beki Sime Vrsaljko, 25, anayelengwa na Liverpool, hataondoka mwezi ujao.. (Corriere dello Sport - via Daily Mirror)


Chelsea huenda wakagonga mwamba kumsajili winga wa Bayer Leverkusen Leon Bailey, 20, mwezi ujao lakini bado wanamtaka kiungo wa kati wa Everton Ross Barkley, 24, na mshambuliaji wa Monaco Thomas Lemar, 22. (London Evening Standard)


Louis Van Gaal: Sijastaafu kufunza soka
Van Gaal astaafu baada ya miaka 26
Lemar anadaiwa kutaka kuhamia Liverpool badala ya kwenda Stamford Bridge ama Arsenal. (Independent)


Arsenal na Liverpool wako katika mazungumzo ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Real Madrid Dani Ceballos, 21. (Diario Gol - via Daily Star)


Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anasema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa asilimia 90 kwamba hataongeza mchezaji mpya katika kikosi chake mnamo mwezi Januari. (BeInSports - via London Evening Standard)


Valencia imekubali dau la £31m kumsajili winga wa Paris St-Germain Goncalo Guedes.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amekuwa katika mkopo katika klabu hiyo ya Uhispania na amevutia Arsenal na Manchester United . (L'Equipe - via Sun)


Arsenal na Manchester City zinamkagua beki wa Burnley James Tarkowski, 25, kwa lengo la kumvutia katika dirisha la uhamisho la mwezi ujao.(Times - subscription required)


Mchezaji anayelengwa na Arsenal na Everton Steven N'Zonzi amedaiwa kuonekana katika uwanja wa ndege wa Gatwick.
Mchezaji huyo wa zamani wa Stoke na Blackburn 29, ameambia Sevilla kwamba anataka kuondoka.. (Sun)


Newcastle wanapigiwa upatu kumsajili mshambuliaji Islam Slimani, 29, kutoka Leicester. (Leicester Mercury)


Klabu hiyo pia imefanikiwa kumtia mkobani kwa mkopo winga wa Chelsea Kenedy, 21, na anatarajiwa kuwasili wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa mwezi ujao. (Daily Mail)


Ajenti wa kiungo wa kati wa Juventus Stefano Sturaro's anasema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye analengwa na Newcastle, huenda akahamia huko mwezi Januari. (Tribal Football - via Newcastle Chronicle)


West Brom itaangazia kumsajili beki wa Middlesbrough Ben Gibson iwapo itamuuza Jonny Evans, 29.
Klabu hiyo hatahivyo inakabiliwa na pingamizi kutoka kwa klabu hiyo ya daraja la kwanza kumnyakua mchezaji huyo mwenye umri wa 24-year-old. (Birmingham Mail)


Kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere, 25, anasema kuwa anataka kusalia katika klabu hiyo na analenga kuichezea Uingereza katika kombe la dunia la 2018 (Sky Sports)


Liverpool itakataa katakata kumuachilia mshambuliaji Daniel Sturridge kuondoka mwezi Januari, na hivyobasi kuweka matumaini yake ya kutaka kuichezea Uingereza katika hali ngumu .
Newcastle, West Ham na Stoke zinamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 (Daily Mail)


Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amempatia Ben Woodburn ruhusa ya kuondoka katika klabu hiyo kwa mkopo.
Leeds United na Sunderland zinamwinda mshambuliaji huyomwenye umri wa miaka 18(Daily Express)


Mkurugenzi wa Inter Milan Walter Sabatini amesisitiza kwamba klabu hiyo haina nia ya kumuachilia Joao Mario, 24, kuondoka mwezi Januari.
Beki huyo amehusishwa na Manchester United and Paris St-Germain. (Independent)


Kipa Claudio Bravo, 34, amesema kuwa ana uhusiano mbaya na mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola lakini anasisitiza kuwa hana mpango wa kuondoka katika klabu hiyo hivi karibuni.(Goal.com) 

" Tuna bahati kumpata Keita " - Mane.

Sadio Mane amesema kwamba Liverpool wana bahati sana kunasa saini ya kiungo Naby Keita kwa msimu ujao wa ligi.

Kiungo huyo wa klabu ya RB Leipzig anatarajiwa kuungana na Mane mwezi Agosti mwakani baada ya kukubali uhamisho wa Pauni Milioni 48 majira ya kiangazi yaliyopita.

Mane ameiambia LFC TV," Ni rafiki yangu. Tena hata sio rafiki, yeye ni kama kaka yangu. Kwasababu muda mwingi huo tunaongea sana, huwa ananiuliza klabu ikoje ? na namuambia ni klabu ya maajabu sana." " Anaijua timu na klabu na anajua Liverpool ikoje. Tunabahati sana kumpata , kwasababu ni mchezaji wa daraja la juu." 

 

 

Spurs ya mtengea dau nono suarez

Tottenham wanaandaa dau nono kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez, kwa mujibu wa Don Balon .

Spurs wanaamini Barcelona watakuwa tayari kumuuza Suarez kwani wanalenga kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann, na miamba hao wa London wameshaanza mazungumzona wawakilishi wa mchezaji huyo.

Lakini mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool anasita kuondoka Camp Nou licha ya kuongezeka ushindani wa namba.


MAN UNITED YACHUANA NA REAL KUMPATA HAZARD
 

Manchester United wamejipanga kupigana vikumbo na Real Madrid kwa ajiliya saini ya Eden Hazard, kwa mujibu wa Sun

Hazard na bosi wa United wamefanya kazi pamoja wakiwa Chelsea, na kufanikiwa kunyanyua taji la Ligi Kuu msimu wa 2014-15.

Na gazeti hilo limedai kuwa United watatoa dau la paundi milioni 90 kwa ajili ya mchezaji huyo msimu ujao.


PSG YAMFUATILIA DIARRA

Paris Saint-Germain wapo kwenye mazungumzo na mchezaji wa zamani wa Chelsea na Real Madrid Lassana Diarra, kwa mujibu wa SFR Sport .

Diarra kwa sasa anaichezea klabu ya Al Jazira ya Falme za Kiarabu, lakini anaweza kuruhusiwa kuondoka kwa uhamisho wa bure Januari.

NAPOLI YAMFUKUZIA KIUNGO WA CITY

Napoli itaanza upya jitihada za kumsajili kiungo wa Manchester City Oleksandr Zinchenko kwenye dirisha la uhamisho Januari, kwa mujibu wa TuttoMercatoWeb .

Zinchenko alijiunga na City mwaka 2016, lakini msimu uliopita alikuwa akitumika kwa mkopo PSV kabla ya kuivutia Napoli majira ya joto.


ATLETICO KUMUUZA GRIEZMANN KWA MAN UNITED

Atletico Madrid wapo tayari kumuuza Antoine Griezmann kwa Manchester United ili kuepuka kumuuza kwa Barcelona ambao ni wapinzani wao, kwa mujibu wa Metro .

 

 

SIMBA YAKIRI KUMUHITAJI ASANTE KWASI, YATUMA BARUA LIPULI


"Ni kweli tunamuhitaji Asante Kwasi kwaajili ya kuja kucheza Simba, na sasa tumepeleka barua rasmi Lipuli FC baada ya TFF kuongeza muda wa usajili.

Nawahakikishia wadau wote wa soka kwamba Kwasi akija Simba atakuwa amekuja kihalali, hawezi kuja kwa njia isiyo halali". Hiyo ni kauli ya mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Zakaria Hanspoppe.

Hanspoppe pia amezungumzia wachezaji walioachwa Simba akithibitisha kumuacha mchezaji mmoja pekee ambapo amesema "Mchezaji aliyeachwa Simba ni Mwanajali peke yake, hakuna mchezaji mwingine aliyeachwa au aliyeongezwa Simba zaidi ya Kwasi". (Azamtv)

0 comments:

Post a Comment