KIUNGO mkabaji wa Yanga raia wa Zimbabwe Thabani Kamusoko, baada ya kuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi miwili, hatimaye leo ameanza rasmi mazoezi ya pamoja na wenzake ambayo yamefanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kamusoko ameonekana kuwa mwenye ari na nguvu zaidi wakati akifanya mazoezi hayo kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara zitakazoendelea kupigwa hivi karibuni baada ya kusimama kwa muda.
0 comments:
Post a Comment