Sadio Mane amesema kwamba Liverpool wana bahati sana kunasa saini ya kiungo Naby Keita kwa msimu ujao wa ligi.
Kiungo huyo wa klabu ya RB Leipzig anatarajiwa kuungana na Mane mwezi Agosti mwakani baada ya kukubali uhamisho wa Pauni Milioni 48 majira ya kiangazi yaliyopita.
Mane ameiambia LFC TV," Ni rafiki yangu. Tena hata sio rafiki, yeye ni kama kaka yangu. Kwasababu muda mwingi huo tunaongea sana, huwa ananiuliza klabu ikoje ? na namuambia ni klabu ya maajabu sana." " Anaijua timu na klabu na anajua Liverpool ikoje. Tunabahati sana kumpata , kwasababu ni mchezaji wa daraja la juu."
0 comments:
Post a Comment