Thursday, December 21, 2017

SPURS YAMTENGEA DAU NONO SUAREZ
ZINAZOHUSIANA

Tottenham wanaandaa dau nono kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez, kwa mujibu wa Don Balon .
Spurs wanaamini Barcelona watakuwa tayari kumuuza Suarez kwani wanalenga kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann, na miamba hao wa London wameshaanza mazungumzona wawakilishi wa mchezaji huyo.

Lakini mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool anasita kuondoka Camp Nou licha ya kuongezeka ushindani wa namba.

MAN UNITED YACHUANA NA REAL KUMPATA HAZARD

Manchester United wamejipanga kupigana vikumbo na Real Madrid kwa ajiliya saini ya Eden Hazard, kwa mujibu wa Sun .

Hazard na bosi wa United wamefanya kazi pamoja wakiwa Chelsea, na kufanikiwa kunyanyua taji la Ligi Kuu msimu wa 2014-15.

Na gazeti hilo limedai kuwa United watatoa dau la paundi milioni 90 kwa ajili ya mchezaji huyo msimu ujao.

PSG YAMFUATILIA DIARRA

Paris Saint-Germain wapo kwenye mazungumzo na mchezaji wa zamani wa Chelsea na Real Madrid Lassana Diarra, kwa mujibu wa SFR Sport .

Diarra kwa sasa anaichezea klabu ya Al Jazira ya Falme za Kiarabu, lakini anaweza kuruhusiwa kuondoka kwa uhamisho wa bure Januari.

NAPOLI YAMFUKUZIA KIUNGO WA CITY

Napoli itaanza upya jitihada za kumsajili kiungo wa Manchester City Oleksandr Zinchenko kwenye dirisha la uhamisho Januari, kwa mujibu wa TuttoMercatoWeb .

Zinchenko alijiunga na City mwaka 2016, lakini msimu uliopita alikuwa akitumika kwa mkopo PSV kabla ya kuivutia Napoli majira ya joto.

ATLETICO KUMUUZA GRIEZMANN KWA MAN UNITED

Atletico Madrid wapo tayari kumuuza Antoine Griezmann kwa Manchester United ili kuepuka kumuuza kwa Barcelona ambao ni wapinzani wao, kwa mujibu wa Metro .

0 comments:

Post a Comment