Uvumi umeanza sasa kuhusu mustakabali wa Zinedine Zidane kuendelea kuwa kocha wa Real Madrid ambapo kiwango chao cha chini msimu huu kimewaacha nafasi ya nne, Pointi 16 nyuma ya vinara Barcelona katika msimamo.
Jarida moja la nchini Italia , La Stampa halina shaka kwamba kuondoshwa katika mashindano ya UEFA ndio itakuwa mwisho wa Zidane katika klabu ya Real.
Wakati huo huo taarifa kutoka Ujerumani zinasema kwamba kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Löw anatajawa kuchukua mikoba ya Zidane endapo kocha huyo ambaye wiki hii amethibitisha kusaini mkataba mpya mpaka 2020 atafukuzwa na Los Blancos.
Imearifiwa kwamba kulikuwa na mawasiliano kati ya Low na Rais wa klabu ya Real Madrid, Florentino Pérez, kabla ya kuajiriwa kwa Zidane mwaka 2016, ambapo mazungumzo hayo hayakuzaa matunda kwasababu ya Low kuonyesha nia yake ya kutoiacha Ujerumani mpaka fainali za kombe la Dunia nchini Urusi mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment