Matheo Antony, Geofrey Mwashiuya, Baruani Akilimali, Juma Mahadhi na Maka Edward ni miongoni mwa wachezaji ambao wamemvutia sana kocha mpya wa Yanga Mwinyi Zahera kinyume na wengi wanavyowachukulia.
Licha ya kutambua mapungufu yao Zahera amesema vijana hao wana vipaji na wataweza kuisaidia Yanga kama wakiimarishwa zaidi.
Wakati Yanga imekwenda Algeria kucheza mchezo wa kwanza wa kombe la Shirikisho dhidi ya USM, Zahera alishangaa kukosekana kwa Matheo, Maka na Baruani lakini akaelezwa majina ya wachezaji hao hayakutumwa CAF.
Kocha huyo ameahidi 'kuwatengeneza' wachezaji hao ili waweze kuisaidia Yanga.
Zahera alisema Matheo, Mwashiuya, Baruani na Mahadhi ni wachezaji wenye kasi ya kuweza kuharakisha mashambulizi langoni kwa mpinzani lakini wana mapungufu kwa kila mmoja tofauti ambayo yeye kama kocha anaweza kuyarekebisha
Zahera ndiye aliyemrejesha Matheo Antony kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga na hakika amedhihirisha ni mchezaji mzuri ambaye anahitaji muda zaidi wa kucheza.
Wachezaji wote wameanza kutumika ipasavyo tangu alipowasili Zahera huku Maka akijihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza baada ya kucheza michezo minne mfululizo.
0 comments:
Post a Comment