Monday, December 18, 2017

Muhispania Sergio Ramos amesema Cristiano Ronaldo ni mchezaji muhimu kwa Real Madrid na ameshakuwa mchezaji bora katika historia ya soka
Nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos amemsifia mchezaji mwenzake Cristiano Ronaldo, akimwelezea kama mchezaji

"ambaye yupo kama hajawahi kutokea".
Mreno huyo ameshinda tuzo ya tano ya Ballon d'Or mapema mwezi huu kwa kuisaidia Los Blancos kutwaa Kombe la Dunia la Klabu.

Ronaldo alifunga goli la ushindi kwenye mechi ya fainali dhidi ya Gremio Jumamosi kutimiza magoli 16 katika mechi 21 msimu huu na Ramos anaamini kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 anastahili tuzo ya mchezaji bora duniani.

"Namba saba wetu ni mshambuliaji wa aina ambayo hatujawahi kuona," alikiambia Telefoot. "Tayari amekuwa gwiji na anatambulika kama mmoja wa wachezaji bora katika historia ya sok. Crstiano Ronaldo ana jukumu muhimu sana kwenye timu na kila mmoja anaheshimu."

Ripoti ziliibuka mwezi uliopita kuwa kulikuwa na ugomvi baina ya Ramos na Ronaldo kwenye chumba cha kubadilishia nguo Bernabeu, jambo ambalo beki huyo wa kati wa Kihispania amekanusha

0 comments:

Post a Comment