Mpya kuhusu Evans.! Kocha wa klabu ya West Brom , Alan Pardew ametaja muda wa mwisho wa mauzo ya beki Johnny Evans ili kuondoa 'fukuto' la usajili la dakika za mwisho za dirisha la usajili.
Arsenal, Manchester City na Manchester United wote wamehusishwa na uhamisho wa beki huyo wa kimataifa wa Kaskazini ya Ireland lakini hakuna ofa rasmi ambayo imewasilishwa. " nitaweka tarehe ya mwisho ya usajili wowote ule .Ninaweza kusema siku tatu au nne kabla ya siku ya mwisho ya usajili kutegemeana na biashara ambayo tumeifanya.Huenda tukafanya biashara katika siku ya mwisho ya usajili."
" sisemi kwamba siwezi kufanya usajili katika siku tatu za mwisho, lakini kama ni usajili mkubwa , wa mmoja wa wachezaji wetu wakubwa na muhimu kwetu na hatukupata muda wa kukamilisha mipango yetu, basi hakuna biashara ya kufanya ." Amesema Pardew.
Saturday, January 13, 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment