Zahera, nampenda sana, Yanga mkimpoteza kocha huyo kwa namna na hali yoyote, mtalaaniwa.
Zahera ni kocha, abahatishi, anafanya anachokijua ambacho ni chenyewe.
Zahera ni kocha bora, katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na pengine Africa kwa ujumla wake, hakuna cha Mzungu, Mwarabu wala Mhindi, hao ni waganga njaa tu, Zahera ndiye mwenyewe, jamaa anajua.
Kocha wangu Abdulmutik Kiduu ni bora, lakini ubora wake niseme tu ukweli, umewazidi hao wengine, kwa Zahera, naona bado hajaufikia.
Nambieni kocha gani katika ugumu wa Yanga angeweza kustahimili na kufanya kazi kwa moyo na mafanikio kama Zahera, awaweke pamoja wachezaji wanaoishi sawa na wale wa timu yangu ya Kijijini Mwiruruma, Mkulima FC, kipato chao, huruma tu za mashabiki wachangechange ndururu kidogo, wawape mithiri ya ombaomba, mkono upate kwenda kinywani, bado wakajituma vile....Uwezo huo anao Zahera tu..... Nilipoiangalia Clip inayomuonesha Zahera akishindwa kuzungumza na kutoa machozi, hakika amini, nami nimetoa machozi.
Tofauti na Zahera, nimetoa machozi kwa furaha, kuona namna mtu huyo anavyoipenda timu yake na kuumia pale anapodhani anaumia kwa ajili ya kuumia au kuumizwa kwa timu yake. Pengine akiwaza nini kingetokea kwa timu yake kama ngawira zingekuwepo za kutosha.
Tangu nizaliwe, huyu Zahera, ni kocha wa kwanza kumshuhudia akifanya kazi katika wakati mgumu, kimaskini, lakini bado akafanya kazi yake kwa moyo na mafanikio.
Wengi niliopata kuwashuhudia, akikosa mshahara miezi miwili, utamsikia ng'ambo ya pili, sauti ya manung'uniko, malalamiko na pengine kejeri, sauti ambayo nadhani husikika hata kwa wafu makaburini, akidai ni ajira, inamlisha na kutunza familia, bila mshahara, hawazi, hafanyi kazi ya kanisa, katika mazingira hayo, wengi wamekuwa wakiingia katika biashara ya kuihujumu timu kwa kuuza mechi.
Zahera, hapana, jamaa ni kocha....Nani anabisha, jifanye kama unajikuna kama hujapofuka.
Lakini pia, tangu nizaliwe, ni mara yangu ya kwanza, kushuhudia kocha akitoa machozi kwa ajili ya timu yake....hii itoshe kukuaminisha kwamba, jamaa anaipenda kazi yake,
anajua nini anakifanya, anaumia kile anachokiamini, ambachoanaamini ndicho, kikawa, au kuwekwa ndivyo sivyo.
Kutoa machozi kwa Zahera mara baada ya mchezo dhidi ya Prisons sababu haswa anazijua mwenyewe, lakini mimi nimehisi katika mambo matatu, nitayasema akiniruhusu.
ni wa pekee sana Zahera katika mpira wa Tanzania na Africa.... Kocha gani, iwe kwa huzuni, furaha, hasira, au kwa namna yoyote ulimshuhudia hapa nchini, akitoa machozi kwa ajili ya timu yake, zaidi ya kupiga picha tu za kumbukumbu.
Hapa amini, Zahera ni kocha, nirudie kusema, Yanga hata kama mkimchoka, msithubutu kumuacha kwa aina walivyoachwa wengine, mpeni heshima yake.
mmfanye kuwa mwanachama wa heshima, wa kudumu, ndani ya timu yenu.
0 comments:
Post a Comment