Winga wa Klabu ya PSG Lucas Moura amesisitiza kwamba atakubali uhamisho wa kuondoka Ufaransa mwezi huu kuhamia Manchester United, kwa mujibu wa taarifa kutoka Telefoot.
Moura amefanikiwa kucheza dakika 72 tu za mechi za ligi kuu ya Ufaransa msimu huu lakini bado ana mpango wa kubaki PSG mpaka mwisho wa msimu.
Vilabu vya La Liga Real Betis na Malaga vyote vimeonyesha nia ya kutaka kunasa saini yake lakini wanakabiliwa na masikitiko makubwa baada ya Jarida la Telefoot kuarifu kwamba Manchester United ndio klabu pekee ambaye Moura atakuwa tayari kuhamia mwezi huu.
0 comments:
Post a Comment