Thursday, January 11, 2018

Straika wa Arsenal Olivier Giroud hana nia ya kuhamia Uturuki au China kwa mujibu wa wakala wake Michael Manuello ambaye ameliambia jarida la Le Figaro:

" Atasikiliza na kuziangalia hizo ofa na baada ya hapo ataamua , kuondoka tu kwasababu ya kuondoka haina maana."

" Lazima ofa iwe na maana na inaongeza kitu kwake . Atakuwa na muda wa kucheza Arsenal, sehemu ya pili ya msimu ni muhimu sana na kuna idadi kubwa sana ya mashindano ya kucheza , hata kama atakuwa anacheza Europa tu."

" Kuondoka kwasababu ya kupata fedha zaidi sio muhimu katika akili yake ."

0 comments:

Post a Comment