kama mambo yalivyo sasa, inaonekana kufikia mwisho wa Januari , Aleix Vidal atavaa tena uzi wa Sevilla.
Kwa miezi kadhaa vilabu hivyo viwili ( Sevilla na Barcelona ) walikuwa wanafanya mazungumzo kuhusu dili hilo huku mchezaji mwenyewe akionyesha nia ya kuondoka na Barcelona wanatak kuuza baada ya kumsajili Philipe Coutinho.
Barcelona walikuwa wanataka kumuuza nje ya nchi hasa baada ya Sevilla kutaka dili la uhamisho wa mkopo na mwishoni mwa msimu kumnunua kwa ada ya Euro Milioni 10 mpaka 12 , ofa ambayo Barcelona wanaiona ndogo.
Matakwa ya mchezai yatakuwa muhimu hasa ukizingatia kwamba hajaridhishwa na ofa kutoka vilabu vya Serie A , AS Roma na Napoli, kurejea katika klabu yake ya zamani ndio chaguo namba moja licha ya Sevilla kutoa ofa ya fedha ndogo.
Akionyesha kiwango bora sana katika maisha yake ya soka katika dimba la Estadio Ramon Sanchez Pizjuan, Vidal alikuwa anacheza beki wa kulia na kufanikiwa kuitwa kikosi cha timu ya taifa ya Hispania.
Anataka kurejesha kile kiwango na Sevilla wanaamini kwamba atapeleka ubora mkubwa zaidi ya usajili wa majira ya kiangazi, Sebastien Corchia
0 comments:
Post a Comment