Thursday, May 17, 2018

Mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann amegoma kuzungumzia kuhusu mustakabali wake baada ya fainali ya kombe la Europa ambapo kocha wake Diego Simeone " atakuwa na furaha kwa uamuzi wowote ule "

Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa alifunga magoli mawili katika ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Marseille na kuisaidia klabu yake kutwaa taji na taji lake la kwanza tangu atue Atletico.

Hata hivyo AG7 anaonekana kumaliza muda wake wa miaka minne ndani ya Atletico na kuhamia Barcelona ambao wameripotiwa kuwa tayari kulipa kiasi cha Pauni Milioni 88

Griezmann amesema," Nafikiri sasa hivi sio muda sahihi wa kuongea kuhusu mustakabali wangu , nataka kusherekea kuhusu kiwango changu na kutwaa taji na nataka kusherekea na mashabiki."

. " Simeone amenifundisha sana na amenifanya kuwa mchezaji mzuri sana na ni matumaini yangu kuendelea kuboresha uwezo wangu kila wakati na katika kila mechi . Nina deni kubwa sana kwa Simeone na wachezaji wenzangu."

Alipoulizwa kuhusu mustakabali wa Griezmann kocha wa Atletico , Diego Simeone amesema," Ni uamuzi ambao atahitajika kuufanya . Chochote atakachoamua nitakuwa na furaha kwasababu ametupa maisha yake yote."

. " Kama akibaki nitafurahi sana na kama akiondoka nitamshukuru sana kwa kila kitu alichotupa ."

" ni matumaini yangu kwamba ana furaha kucheza katika klabu yetu, Amecheza fainali tatu na sisi na ameshinda fainali mbili . Na sasa tutacheza Super Cup ya UEFA , kwahiyo huenda akacheza fainali nne na sisi."

. " Kwa hiyo kwa upande wa kimichezo hatuko mbali na vilabu ambavyo vina nguvu zaidi yetu."

0 comments:

Post a Comment