Thursday, November 8, 2018

Klabu ya Barcelona imethibitisha kuwa Kiungo wao wa Kimataifa wa Brazil, Philippe Coutinho atakuwa Nje Kwa muda wa wiki Mbili Mpaka tatu baada ya kupata majeraha ya mguu.

Coutinho anatarajia kukosa baadhi ya mechi za timu yake ya Taifa ya Brazil Ambayo itashuka Dimbani kucheza Dhidi ya Cameroon  na Dhidi ya Uruguay (November 16 na 20).

Ikiwa atarejea mapema Kwa muda wa wiki Mbili basi atakuwepo Katika Kikosi cha Barcelona kitakachoivaa Atletico Madrid kwenye mechi ya Laliga Siku ya November 24, lakini akikaa Mpaka wiki tatu atarejea Katika mechi ya UEFA Champions League Dhidi ya PSV November 28.

Lakini Barcelona Katika Taarifa yao wamesema kuwa Mchezaji huyo ikiwa atachelewa kupona basi huenda akakosekana mwezi huu November Wote.

0 comments:

Post a Comment