Jeshi la Polisi katika eneo la Merseyside, limethibitisha kupokea taarifa za kutishiwa kifo dhidi ya mlinda lango wa Liverpool, FC Loris Karius
Kipa huyo analaumiwa kwa kucheza fyongo katika Mchezo wa Fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya
Karius mwenye umri wa miaka 24 pamoja na familia yake wamekuwa wakipokea vitisho baada ya makosa mawili aliyoyafanya yaliyowasadia Real Madrid kupata ushindi wa mabao 3 kwa1
Maafisa wa Jeshi la Polisi wamesema vitisho vyovyote vinavyotolewa kupitia mitandao ya kijamii lazima vitachunguzwa.
0 comments:
Post a Comment