Tuesday, June 19, 2018

Klabu ya Atletico Madrid ya Hispania imewaongezea mikataba wachezaji wake wawili mshambuliaji Antoine Griezmann na beki wa kati Lucas Hernandez.

Mshambuliaji na mfaransa Griezmann mwenye umri wa miaka 27, ameongeza mkataba mpya utakaomfanya kubakia klabuni hapo hadi mwaka 2023.

Beki aliyeibukia katika Academy ya klabu hiyo ambaye pia ni mfaransa Hernandez mwenye umri wa miaka 22, ameongeza mkataba mpya utakaombakiza klabu hapo hadi mwaka 2024.

0 comments:

Post a Comment