Monday, July 23, 2018


Klabu ya Biashara United ya Mara leo imewatangaza wachezaji wanne ambao imewasajili kutoka vilabu tofauti ili kuendelea kujiimarisha kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajiwa kuanza Agosti 22, 2018.

Wachezaji hao ni Lambele Jerome kutoka Lipuli, Yohana Moris aliyekuwa Mbeya City, Frank Sekule kutoka Dodoma FC na Daniel Manyenye kutoka Toto Africans.l

Meneja wa timu hiyo Aman Josiah amesema kuja kwa wachezaji hao kutaendelea kuimarisha timu hiyo na hivyo kuingia katika ligi kuu kiushindani na si kushiriki.

0 comments:

Post a Comment