Monday, July 23, 2018

Kaimu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Clement Sanga, ametangaza kujiuzulu wadhifa wake katika klabu hiyo leo Julai 23

Sanga amejiuzulu wadhifa huo kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri baina yake na viongozi wenzake ndani ya klabu hiyo ikiwemo wale wa Kamati ya Utendaji kueleza hana ushirikiano mzuri

Mbali na kukosa maelewano, Sanga amedai kuwa kuna habari ameiona inayohamasisha watu kumvamia yeye na familia yake kwa mapanga nyumbani kwake

Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Charles Boniface Mkwasa naye amethibitisha rasmi kuachia ngazi leo kutokana na kusumbuliwa na masuala ya kiafya

0 comments:

Post a Comment