Daniel Sturridge amesisitiza kwamba atabaki Liverpool kwa msimu mpya wa Ligi kuu ya soka ya Uingereza na kupigania nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza chini ya Jurgen Klopp.
" Najiona kubaki Liverpool , na matumaini ya kuwa kikosini wiki hadi wiki . Maandalizi ya msimu mpya yanaendelea vizuri kwahiyo kwangu mimi ni kujituma tu. "
" Nina hamu sana na msimu mpya na najisikia vizuri kurejea klabuni "
Daniel Sturridge raundi ya pili ya msimu uliopita alicheza kwa mkopo katika klabu ya West Brom ambayo ilishuka daraja.
0 comments:
Post a Comment