Thursday, July 26, 2018

Mambo yanazidi kuiendea vibaya klabu ya Yanga baada ya beki wao wa kulia Hassan Kessy kuthibitisha kwamba anaondoka kwenye klabu hiyo baada ya kushindwa kuafikiana mkataba mpya na timu hiyo.

Kessy ameripotiwa kwamba yuko mbioni kujiunga na mabingwa wa zamani wa Zambia, Nkana Red Devils na sasa yupo nchini humo kukamilisha taratibu za usajili.

Awali Kessy alitarajiwa kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia Yanga lakini pande hizo mbili hazikuweza kufikia muafaka.

0 comments:

Post a Comment