David Luiz amesisitiza kwamba hana mpango wa kuondoka Chelsea , kwa kuelezea 'mahaba' yake ya falsafa nzuri ya kocha Maurizio Sarri.
Luiz mwenye umri wa miaka 31 amepewa nafasi ya maisha mpya ndani ya Stamford Bridge baada ya kuonekana kutoka mlango wa nje wa Chelsea chini ya Antonio Conte.
Luiz ambaye alirejea darajani kutoka Paris Saint-Germain kwa dau la Pauni Milioni 32 mwaka 2016 amesema," Nilirejea Chelsea kubaki hapa."
" Nilipochukua uamuzi wa kurudi Chelsea kutoka Paris ilikuwa ni kwa ajili ya kutwaa taji la Ligi kuu ya Uingereza na kufanya kitu kipya tena na Chelsea, kwahiyo nina furaha sana hapa ."
" Naipenda Falsafa ya Sarri, tunacheza zaidi juu ya kiwanja na kumiliki zaidi mpira kwa staili ya kiufundi , anajaribu kila siku kutusaidia kuelewa falasafa yake."
0 comments:
Post a Comment