Everton watafanya mazungumzo ya kuboresha mkataba mpya wa Golikipa Jordan Pickford pindi kipa huyo atakaporejea klabuni wiki hii.
Pickford alikuwa kwenye mapumziko ya muda mrefu baada ya kuonesha kiwango kizuri katika fainali za kombe la Dunia nchini Urusi.
Taarifa kutoka Sky Sports zinasema kwamba Chelsea wameonesha nia ya kutaka kumsajili Golikipa huyo namba moja wa Uingereza ili kuziba pengo la Golikipa ambaye anahusishwa na kuondoka darajani, Thibaut Courtois.
Pickford alisaini kwa klabu hiyo ya jijini Merseyside majira ya kiangazi yaliyopita kwa dau la Pauni Milioni 30 kutoka Sunderland.
0 comments:
Post a Comment