Monday, July 30, 2018

Haruna Niyonzima akiwa bado kwao Rwanda na kuchelewa kujiunga na kikosi cha Simba kwenye kambi ya Uturuki, Rais wa Simba Salim Abdallah amesema Niyonzima hatoweza tena kwenda Uturuki kwa sababu muda umekwenda.

Salim amesema wanatarajia kumhoji Niyonzima kwa kosa la kukaa kimya hadi sasa.

"Haruna ni mchezaji wa Simba, tulimpa ruhusa maalum ya mapumziko na matibabu kule kwao Rwanda."

"Tarehe ambayo alitakiwa kurudi Haruna ilikuwa ni July 20 ili aweze kuungana na wenzake, hata passport yake ina visa ya Uturuki lakini kwa sababu ambazo tumeshindwa kuzifahamu hadi sasa Haruna hajajiunga na timu, mwaka jana alikosa pre-season hata performance yake haikuwa nzuri kwa sababu ya kukosa pre-season na kukaa pamoja na wenzake."

"Mwaka huu tena anakutana na tatizo hilohilo, sisi kama uongozi tunajaribu kuangalia kwa nini Haruna hajajiunga na timu kwa ajili ya pre-season."

"Zipo taratibu na namna ya kufanya, kama ni makosa basi tutamwadhibu kwa mujibu wa taratibu zetulakini tutampa nafasi ya kujieleza kwa nini hajajiunga na timu."  Rais wa Simba Salim Abdallah (try again)

0 comments:

Post a Comment