Wakati kikosi cha Manchester United kikiwa tayari katika mji wa Los Angeles nchini Marekani kwa ajili ya Kujiandaa na msimu mpya, nyota wa timu hiyo raia wa Chile Alexis Sanchez amebaki nchini Uingereza kutokana na kunyimwa visa ya kuingia Marekani baada ya kukutwa na hatia ya ukwepaji kodi pindi alipokuwa nchini Hispania :
Mwezi February mwaka huu Sanchez alikutwa na hatia ya ukwepaji kodi wa kiasi cha £885, 000 kipindi alipokuwa akichezea Fc Barcelona na alihukumiwa kwenda jela kwa muda wa miezi 16 lakini mchezaji huyo alikiri kosa hilo na kukubali kulipa kiasi hicho na faini juu :
Ikiwa nchini Marekani, Manchester United itacheza dhidi ya Club America, San Jose Earthquakes, Ac Milan, Liverpool, Real Madrid kisha kumaliza na Bayern Munich kabla ya kucheza mechi yao ya kwanza ya ligi dhidi ya Leicester city
0 comments:
Post a Comment