Mwanasoka bora chipukizi katika michuano ya kombe la dunia Kylian Mbappe ametoa msaada wa fedha zote alizolipwa kutokana na ushiriki wake katika michuano hiyo - kiasi cha $550,000 (takribani billioni 1.3) ambazo zinatokana na malipo ya posho pamoja na bonasi ya kushinda kombe la dunia .
Fedha hizo amezitoa kama msaada kwenye kituo ambacho kinatoa bure huduma za michezo kwa watoto wasio na uwezo wa kumudu gharama pamoja na wanamichezo watoto wenye ulemavu nchini Ufaransa.
0 comments:
Post a Comment