Tuesday, July 31, 2018

Rapa Nicki Minaj amechukua nafasi ya KANYE WEST Katika orodha ya wasanii walioingiza nyimbo nyingi zaidi kwenye chati za Billboard Hot 100.

Kupitia kazi mpya ya rapa 6ix9ine Ft Nicki Minaj "FeFe," inayoshikilia nafasi ya NNE kwenye Billboard Hot 100,  Nicki Minaj amekuwa na nyimbo 93 kwenye chati hizo huku Kanye West akiwa na nyimbo 92.

Kwenye orodha hio yenye heshima kubwa sasa NICKI MINAJ Yupo nyuma ya wasanii Glee Cast wenye nyimbo (207), Drake ameingiza nyimbo (186), Lil Wayne ana nyimbo (138), Elvis Presley anazo (108) na JAY-Z ameingiza nyimbo (98) kwenye chati za billboard hot 100.

Kwa wasanii wa kike wa RAP, Hii ni nyimbo ya 17 iliyoingia kwenye top ten za chati hio, Minaj anaongoza kwenye Rekodi hii akifwatiwa na Missy Elliott mwenye nyimbo 9.

Album mpya ya Nicki Minaj 'Queen' inatoka August 10 2018,

0 comments:

Post a Comment