Mshambuliaji mpya wa Juventus aliyesajiliwa kutoka Real Madrid Cristiano Ronaldo kwa ada ya uhamisho inayotajwa kuwa Euro milioni 112 Mwezi Julai amejiunga na wachezaji wenzake na kuanza mazoezi Jana Jumatatu.
Taarifa kutoka Klabuni hapo zimeeleza kuwa Sambamba na Cristiano Ronaldo kuanza mazoezi pia wachezaji wengine kama Gonzalo Higuain, Rodrigo Bentancur, Paulo Dybala, Douglas Costa na Juan Cuadrado nao wamerejea.
Juventus wanatarajia kucheza na Real Madrid katika michuano ya ICC siku ya Jumamosi ukitanguliwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya MLS All-Star lakini bado haijawekwa wazi kama Ronaldo atakuwa fiti kucheza mchezo huo.
Hata hivyo Ronaldo anategemewa kuanza kucheza mchezo wake wa kwanza Agosti 18 dhidi ya Chievo.
0 comments:
Post a Comment