Sunday, September 23, 2018

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kwamba jeraha alilopata beki Virgil Van Dijk sio kubwa na atakuwa sawa sawa.

Beki huyo wa kimataifa wa Uholanzi aliumia kwenye mechi dhidi ya Soton na nafasi yake kuchukuliwa na Joel Gomez kipindi cha pili.

Klopp aliulizwa baada ya mechi kuhusu VVD, “ Tayari alikuwa na mchubuko kwenye mbavu kabla ya mechi dhidi ya PSG , na ameumia tena sehemu ile ile leo.”

  “ Sio kitu kizuri lakini sio jeraha kubwa. Matumaini yangu kwamba atakuwa sawa kabisa. Sijasikia bado kitu chochote tofauti.”

0 comments:

Post a Comment