Monday, September 17, 2018

Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, ameibuka na kuwapiga dongo watani zake wa jadi kuwa mpira waliocheza dhidi ya Stand United jana walitamani mechi iishe mapema.

Amefunguka hayoe na kudadavua  kuwa Yanga haikucheza mpira wa kifundi na badala yake walizidiwa kimbinu  nyingi na Stand United hali iliyopelekea wakoswekoswe na mabao kadhaa.

Alienda mbali zaidi na kueleza kuwa Yanga waliona hali ngumu na kuanza kuomba mechi iishe haraka ili wasalie na matokeo yao ambapo walikuwa wanaongoza.

Manara aliamini kuwa #StandUnited wangeweza kusawazisha magoli kwenye mchezo huo baada ya Alex Kitenge kufunga bao la tatu, kutokna na alichokiona yeye kwamba watani zake walianza kuelemewa na mbinu za Stand United.

Mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Taifa jana, Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-3. huku mzigo wa lawama akibebeshwa kipa wake Mkongo Klaus Kinzi juu ya mabao aliyofungwa.

0 comments:

Post a Comment