Monday, September 17, 2018

Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” itacheza mchezo wake wa kutafuta tiketi ya kufuzu Afcon dhidi ya Cape Verde Oktoba 12, 2018 na mchezo wa marudiano utachezwa Uwanja wa Taifa Oktoba 16, 2018.

TFF kwa kushirikiana na Wadhamini wa Taifa Stars Bia ya Serengeti Premium Lager tunafanya utaratibu wa usafiri utakaoipeleka na kuirudisha timu ya Taifa kulingana na ratiba ya michezo hiyo ilivyokaa.

Utaratibu wa Kambi/Kikosi Walimu watauzungumza ambao utazingatia umuhimu wa mchezo,tarehe za kuondoka na tarehe za michezo yote miwili.

Unafanyika utaratibu wa kusafiri na mashabiki wa timu ya Taifa ambao watachangia gharama kidogo.

Tumekuja na Hashtag itakayotumika katika safari yetu ya kutupeleka Cameroon kwenye fainali hizo za mwakani #AfconCameroon2019ZamuYetu
Rai yetu kwa Vyombo vya Habari tuungane pamoja kwakuwa ni sehemu muhimu katika safari hiyo ya kwenda Cameroon,Wadau mbalimbali tuungane pamoja Tanzania ni yetu,Taifa Stars ni timu yetu.

Msimamo ulivyo mpaka sasa tunayo nafasi ya kwenda Cameroon kwenye Fainali za Afcon.

Uganda wanaongoza wakiwa na alama 4 ,Lesotho na Tanzania wana alama 2 na Cape Verde wakiwa na alama 1.

0 comments:

Post a Comment