Tuesday, September 25, 2018

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amempoteza kabisa kocha wa zamani wa timu hiyo, Mzambia George Lwandamina kwa kuweka rekodi ya aina yake katika Ligi Kuu Bara.

Zahera, mwenye uraia wa DR Congo na Ufaransa, amejiunga Yanga kwa kuchukua mikoba ya Mzambia huyo ambaye aliamua kurejea kwenye timu yake za zamani ya Zesco United ya nchini kwao.

Kocha huyo ameweka rekodi hiyo ya aina yake katika mechi tatu za msimu kwa kuweza kushinda zote tofauti na Lwandamina katika msimu uliopita.

Zahera mpaka sasa ameweza kuiongoza Yanga kushinda mechi tatu na kupata pointi tisa ikiwa sawa na dakika 270, tofauti na Lwandamina ambaye alishinda mechi moja katika mechi tatu za kwanza na kutoka sare mbili.

Yanga chini ya Zahera katika msimu huu imefanikiwa kumfunga Mtibwa Sugar mabao 2-1 kisha Stand United mabao 4-3 kabla ya Jumatano ya wiki iliyopita kuwatungua Coastal Union bao 1-0.

Kwa upande wa Lwandamina, mechi yake ya kwanza msimu uliopita alianza kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Lipuli halafu akatoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Maji Maji kabla ya kuwafunga Njombe Mji bao 1-0 katika mechi zake tatu za kwanza.

0 comments:

Post a Comment