Baada ya ushindi wa jana dhidi ya Singida United, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kwenda mkoani Morogoro kuweka kambi kuelekea mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa uwanja wa Taifa Jumapili ijayo, Septemba 30, imefahamika
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ametaka timu hiyo iweke kambi mahali penye utulivu kabla ya mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu.
Jana baada ya mchezo dhidi ya Singida United, Kamati ya Mashindano inayoongozwa na Hussein Nyika ilitarajiwa kukutana kupitisha maamuzi ya kambi hiyo.
Inaelezwa Kocha Zahera amependekeza Yanga irudi mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo huo.
Zahera amevutiwa na mandhari ya mkoa wa Morogoro ambako waliweka kambi kabla ya mchezo dhidi ya USM Alger mwezi August.
Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 ilipotoka Morogoro na kuivaa USM Alger kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho uliopigwa uwanja wa Taifa August 19, 2018.
Miaka yote Yanga imekuwa na kawaida ya kuweka kambi nje ya jiji kabla ya mchezo dhidi ya Simba.
0 comments:
Post a Comment