Saturday, September 22, 2018

Uongozi wa Yanga umegomea kubadilishwa kwa ratiba ya mechi yao dhidi ya JKT Tanzania mchezo uliokuwa uchezwe siku ya Jumatano ya September 26. Yanga wamedai hawatambui mabadiliko ya mechi yao kwani wao hawajaomba kusongezwa mbele kwa mchezo huo na kama Simba waliomba basi wangesongeza mechi ya Simba na kuiacha mechi yao kama kawaida kwani mwalimu alikuwa amejiandaa na ratiba ya mechi hizo.

Jana bodi ya ligi iliahirisha michezo miwili inayowahusu Simba na Yanga mchezo namba 63 kati ya JKT Tanzania dhidi Yanga uliokuwa uchezwe siku ya Jumatano ya September 26 na mchezo namba 64 kati ya Simba na Biashara uliokuwa Uchezwe Alhamisi ya September 27 ili kuzipa muda timu hizo kujiandaa na mchezo wa watani wa jadi siku ya Jumapili ya September 30.

Simba bado hawajatoa msimamo wake yawezekana wefurahishwa na taarifa hii. Ili wajiandae vizuri kwa ushindi kutokana na kuwa na mwenendo mbovu katika mechi mbili zilizo pita.

0 comments:

Post a Comment