Thursday, October 18, 2018

Aliyekuwa kocha msaidizi wa Simba Masoud Djuma amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuifundisha AS Kigali inayocheza ligi kuu ya Rwanda.

Masoud amechukua nafasi ya Eric Nshimiyimana ambaye amejiuzulu kuifundisha klabu hiyo.

Masoud ameondoka Simba baada ya kuwa kocha msaidizi kwa takribani mwaka mmoja lakini hivi karibuni ilitoka taarifa kuwa pande zote mbili zilikubaliana kuvunja mkataba.

Kabla ya kujiunga na Simba Masoud alikuwa kocha mkuu wa Rayon Sports ya Rwanda na aliondoka akiwa ameipa ubingwa wa Rwanda 2016/17.

Amepata kazi fasta baada ya kurejea Rwanda huenda kwa sababu ya kufanya vizuri kwenye ligi kabla hajaondoka lakini pia uzoefu wake kwenye ligi hiyo kwa maana anajua afanye nini ili AS Kigali ifanye vizuri.

0 comments:

Post a Comment