Kupitia mtandao wa instagram harmonize ameshangaza watu baada ya kupost picha akiwa na haromrapa na kumuandikia ujumbe mzito wenye kutia noyo
Harmonize kaandika hivi "Mwiko kukata Tamaa ama kukatishwa na mtu yeyote yule katika safari yako ya mafanikio hii safari ni ndefu sana....!!! Utakutana na changamoto nyingi mno....!!! yakiwemo matusi, dharau, uonevu, chuki,
namengine kibao ila pale utakapokubali kukata tamaa ama kukatishwa utakuwa umewavunja moyo watu wengi sana....!!!! (1) familia yako (2) ndugu jamaa na marafiki( 3) hata wale wachache waliokuwa wanakutia Moyo na motisha uongeze jitihada nawengine wengi mno....!!! Itakuwa umewavunja moyo ...!! lakini pia M/mungu ni waajabu na hajawahi kukosea katika hii Dunia kila alifanyalo lina maana
Kubwa sana..!!! Wenda kawaumbe Binadam wengine kwa mfano wako nikiwa namaana mnafanana ambalo ni jambo la heri na baraka 🙏 so ukikata tamaa nao pia utakuwa umewaangusha jitihadazako, maarifa, kuzishinda changamoto ndio njia peke inaweza kuleta faraja kwa wengi wanao kuzunguka zingatia hili 👉 #MaishaNiKombolela....!!! God bless my twins brothers 🙏🙏"
Harmorapa amerudi insta baada ya kuka kimya kwa mda mrefu bila kurusha pisha , lakini amekanusha madai ya kufunga harusi.
Anadai video zinazo sambaa ni vipande vya movie inakuja hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment