Chelsea wameingia vitani dhidi ya Internazionale, Roma na Sampdoria kuwania saini ya kiungo wa Brescia , Sandro Tonali, ambaye amebatizwa " Pirlo Mpya " kutokana na kipaji chake cha kuchezesha timu na staili ya nywele.
Brescia walikataa ofa kutoka Roma na Sampdoria yenye thamani ya Pauni Milioni 10.5 majira ya kiangazi ambapo Chelsea wenyewe wameamua kupandisha dau zaidi mpaka kufikia Pauni Milioni 17.5 kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 18
Lakini Inter Milan wameamua kuwasilisha ofa yao mwezi Januari na kumuachia kiungo huyo abaki Brescia kwa mkopo kwa miezi 18.
0 comments:
Post a Comment