Baada ya kwenda nchini Afrika kusini wachezaji wa Azam FC kwaajili ya matibabu Frank Domayo na Paul Peter ,Domayo amerejea nchini jana na taarifa ya daktari inasema kuwa hatafanyiwa upasuaji ila atafanyiwa tiba mbadala itakayomfanya awe nje ya Uwanja kwa muda wa miezi miwili huku Peter akibaki nchini humo kwaajili ya kufanyiwa upasuaji.
Domayo na Peter wamepata majeraha ya goti, Domayo aliumia hivi karibuni akiwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ iliyokuwa ikifanya maandalizi ya kuvaana na Cape Verde octoba 12 mwaka huu, huku mshambuliaji peter naye akiumia miezi michache iliyopita akiwa na timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes
Afisa habari wa Klabu hiyo Jaffar Iddi amesema kuwa wamempokea jana mchezaji wao Domayo akitokea Afrika kusini ambapo ripoti ya daktari inasema kuwa hatafanyiwa upasuaji huo na atatibiwa hapahapa nchini ila Peter atafanywa upasuaji.
Jaffary ameongeza kuwa wanatambua mchango wa wachezaji hawa ndani ya kikosi chao na wanawaombea wapone haraka ili warudi kwenye Timu kwaajili ya kuendelea na majukumu yao.
0 comments:
Post a Comment