Mshambuliaji Obrey Chirwa raia wa Zambia yuko nchini kumalizana na Yanga, klabu aliyoitumikia kwa misimu mitatu kabla hajaondoka mwanzoni mwa msimu huu, imefahamika.
Chirwa aliyeifungia Yanga mabao 32 katika misimu yake mitatu, alitimkia Misri kujiunga na timu ya Nogoom El Mostakbal FC inayoshiriki ligi daraja la pili.
Hata hivyo imeelezwa kuwa Chirwa kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wake na timu hiyo ambayo inadaiwa kushindwa kumlipa fedha zake za usajili.
Mwezi uliopita ziliibuka taarifa kuwa Chirwa aliwasiliana na uongozi wa Yanga akiomba arejee klabuni hapo baada ya kushindwana na Nogoom.
Leo Chirwa alikuwepo uwanja wa Taifa kushuhudia mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya Yanga dhidi ya Alliance Fc akiwa sambamba na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga Hussein Nyika pamoja na Kaimu Katibu Mkuu Omary Kaya.
Chirwa anatarajiwa kurejea Jangwani wakati wa dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa mwezi ujao.
0 comments:
Post a Comment