Friday, October 26, 2018

Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limeikatalia La Liga ombi la kutoa kibali ili baadhi ya michezo ya ligi kuchezwa nchini Marekani na kusisitiza mechi za ligi ya ndani lazima zichezwe ndani ya mipaka ya nchi husika.

Kamati ya FIFA imekutana leo Ijumaa kuzungumzia juu ya maombi ya La Liga yaliyowasilishwa na Rais wa La Liga Javier Tebas.

La Liga walikuwa wanataka mchezo wa Girona vs Barcelona wa tarehe 26, January uchezwe Miami. Hatua hii ilikuja baada ya La Liga kusaini mkataba wa miaka 15 na kampuni ya Relevent Sports ya US.

“Nalipinga jambo hili kwa nguvu zote, na nawanyima kibali cha mchezo Girona vs Barca kuchezwa Miami.”  alisema Rais wa FIFA Gianni Infantino.

“Michezo rasmi ya ligi lazima ichezwe kwenye mipaka ya nchi husika, FIFA imeweka wazi uamuzi wake juu ya suala hili.”

0 comments:

Post a Comment