Friday, October 26, 2018

Klabu ya Tottenham itaendelea  kutumia Uwanja wa Wembley kama Uwanja wao wa nyumbani Kwa mechi zote ambazo wao watakuwa ni Wenyeji wa Mchezo  mpaka mwakani ambapo ndio uwanja wao binafsi "White Hart Lane Stadium" utafunguliwa rasmi..

Hili limekuja baada ya kutokamilika Kwa Uwanja wa uwanja wao Ambao upo Katika ujenzi wa kuutanua ili kuongeza idadi ya watazamaji, Mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy Amethibitisha kuwa wameongeza Siku za kuutumia Uwanja wa Wembley kama ndio nyumbani kwao Mpaka mwanzoni mwa mwaka 2019.

Mapema walitangaza kuwa rasmi wataanza kuutumia Uwanja wao binafsi mwezi huu Oktoba lakini imekuwa tofauti na Siku zimezidi kupelekwa Mbele, Levy amesema kuwa kufikia Disemba White Hart Lane itafunguliwa..

0 comments:

Post a Comment