Kocha Joachim Low ameweka rekodi mpya ya kuwa kocha ambaye ameifundisha timu ya taifa ya Ujerumani mechi nyingi kuzidi makocha waliopita.
-Mechi ya Jana ya UEFA Nations League dhidi ya Uholanzi, Low alikuwa akiiongoza Ujerumani katika mechi ya 168 yeye akiwa kama kocha mkuu akianza Rasmi kibarua chake mwaka 2006 akichukua mikoba ya Jurgen Klinsmann ambaye hapo nyuma alikuwa akimsaidia wakiiongoza Ujerumani kushika nafasi ya tatu katika kombe la Dunia.
Low 58, kabla ya kuvunja rekodi hiyo ilikuwa ikishikiriwa na Marehemu, Sepp Herberger ambaye alikuwa kocha mkuu wa Ujerumani katika mechi 167..
Herberger Alifariki dunia akiwa na miaka 80 Siku ya Aprili 28,1977, katika zama za kucheza soka lake kaichezea Ujerumani katika mechi tatu tu na kufunga goli Mbili kati ya mwaka 1921-1925.
Pia Herberger akiwa kama kocha mkuu wa Ujerumani ameiongoza kutwaa kombe la Dunia mwaka 1954, kawa kocha kati ya mwaka 1936-1942, (1945-46 alikuwa kocha mkuu wa Frankfurt) akarejea tena kipindi ikiitwa West Germany mwaka 1950-1964....Pia aliwahi kuwa kocha msaidizi kati ya mwaka 1932-1936.
Low ameisaidia Germany kutwaa kombe la Dunia mwaka 2014, pia kaisaidia kushika nafasi ya pili katika Euro 2008, Nafasi ya tatu ya kombe la Dunia 2010.
0 comments:
Post a Comment