Kamati ya saa 72 ya shirikisho la soka Tanzania (TFF) itakutana kujadili matukio ya utovu wa nidhamu yaliyojitokeza kwenye mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba dhidi ya Yanga uliopigwa Jumapili iliyopita kwenye uwanja wa Taifa.
Akizungumza jana jijini Dar es salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura, alisema kamati ya saa 72 itakutana muda wowote ili kujadili matukio hayo.
Wambura alisema kuwa wachezaji watakaojadiliwa katika kikao hicho ni Pascal Wawa, James Kotei wa Simba, huku kwa upande wa Yanga ni mshambuliaji, Heritier Makambo na Andrew Vicent "Dante" na hiyo imetokana na 'video clips' zinazosambaa mitandaoni zinazoonyesha walifanya vitendo visivyo vya kiuanamichezo. "Hizi 'video clips' zinazotembea mitandaoni ndizo zinazotukutanisha, ila siwezi kuzungumzia hatua zitakazochukuliwa hadi kamati itakapokutana," alisema Wambura.
0 comments:
Post a Comment