Beki wa timu ya taifa ya Hispania, Marcos Alonso amesaini Mikataba mpya wa miaka mitano Kuendelea kuitumikia Klabu yake ya Chelsea.
Beki huyo ambaye ni zao lililotengenezwa na Real Madrid akianzia Academy Mpaka Senior team, pia ni beki wa Zamani wa Bolton Wanderers, Sunderland na Fiorentina, na Sasa Chelsea mkataba huo mpya utafikia kikomo mwaka 2023...
Alonso 27, Alijiunga na the blues Kwa Dau la £24m kutoka Fiorentina mwezi Agosti wa mwaka 2016 na tokea hapo amekuwa ni Mchezaji tegemeo Katika Kikosi cha Chelsea yeye mwenyewe akijihakikishia Nafasi baada ya kuwa na uwezo mzuri wa kukaba,kupandisha mashambulizi,kutengeneza Nafasi na hata kufunga Magoli...Kaichezea Chelsea mechi 73 na kufanikiwa kufunga Magoli 14 na Assist 7.
Kwa mujibu wa vyanzo, tayari beki huyo alikuwa akinyatiwa na Vilabu vikubwa Barani Ulaya, vikiwemo Real Madrid na FC Barcelona, Lakini kocha mkuu wa Chelsea Maurizio Sarri amemshawishi mhispania huyo kusaini mkataba mpya klabuni hapo.
0 comments:
Post a Comment