Friday, October 12, 2018

Marquinhos huenda akafanya maamuzi ya kuondoka PSG kama akiendelea kuchezeshwa namba 6 na kocha wake , kwa mujibu wa taarifa kutoka Le10Sport.

Thomas Tuchel amemtumia Mbrazil huyo katika eneo la kiungo mara kwa mara huku Marquinhos mwenyewe anaamini kwamba beki wa kati ndio namba yake sahihi.

Wawakilishi wa Marquinhos wamefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Michezo wa PSG Antero Henrique  kuhusu swala hilo, na beki huyo ataamua kuondoka endapo hali hiyo itaendelea.

0 comments:

Post a Comment