Wednesday, October 31, 2018

Klabu ya Tottenham Hotspur inatazamiwa kukopa pauni Milioni 237 ili kuweza kukidhi gharama  zilizoongezeka katika ujenzi wa uwanja wao mpya.

Katika taarifa yao waliyoitoa ijumaa usiku klabu iliweka wazi kuwa uwanja wao hautakuwa tayari hadi mwaka 2019 tofauti na ilivyotegemewa hapo awali kuwa ungekuwa tayari mwishoni mwa mwaka huu.

Pia timu hiyo ya jijini London ilitangaza deni lao la pauni milioni 366 linategemewa kuongezeka kufikia pauni 600 Millioni.

Mwezi Mei mwaka 2017 klabu ilitangaza mkakati wa miaka mitano wa kiasi cha pauni 400 Millioni kwa ajili ya uwanja wao, wakishirikiana na benki tatu Bank of America Merrill Lynch, Goldman Sachs pamoja na HSBC.

Kwenye taarifa ya ijumaa klabu ilithibisha sasa uwanja huo utakuwa na thamani ya pauni milioni 637 ikiwa ni ongezeko la pauni 237 Millioni toka ile pauni Milioni 400 ya mwanzo.

Tottenham kwa sasa wanatumia uwanja wa Wembley kwa mechi zao za nyumbani wakisubiri ujenzi katika uwanja wao wa White Hart Lane kukamilika.

Walipanga kufungua uwanja wao mpya kwenye mechi ya ligi Septemba 15 dhidi ya Liverpool ila haikuwezekana na kubadili hadi Disemba 15 kwenye mechi yao dhidi ya Burnley ila nayo imesogezwa mbele na sasa mategemeo ni kuufungua uwanja huo Januari 13 2019 kwenye mechi yao dhidi ya Manchester United.

0 comments:

Post a Comment