Mshambuliaji wa klabu ya Genk ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mbwana Samatta ameendeleza moto wa kupachika mabao katika michuano ya 'Europa League' usiku wa jana.
Samatta amepachika mabao mawili na kuisaidia Genk kuondoka na alama tatu kwa kuichapa Besiktas mabao 4-2 katika uwanja wake wa nyumbani mjini Instanbul, Uturuki.
Samatta alifunga mabao yake dakika za 23 na 69, akimfunga mlinda mlango, Loris Karius aliyejiunga Besiktas kwa mkopo akitokea Liverpool msimu huu. Karius alisimama langoni mwa Liverpool katika fainali ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid mwezi Mei mwaka huu.
Katika mchezo huo Mbwana Samatta aliibuka nyota wa mchezo. Kutokana na mabao mawili aliyofunga na mchango wake katika moja ya bao la genk.
Genk wanaongoza kundi L wakiwa na point 6 wakifuatiwa. Samatta amecheza jumla ya mechi 8 za ueropa league na kufanikiwa kufunga goli 9.
0 comments:
Post a Comment