Imeripotiwa kuwa Klabu ya Yanga SC imeanza mazungumzo na beki, Mnyarwanda Abdul Rwatubyaye ikiwa ni harakati zao za kuhakikisha wanaipata saini yake katika dirisha dogo linalofunguliwa mwezi ujao.
Rwatubyaye anaichezea Rayon Sports ya Rwanda aliivutia Yanga wakati timu hizo mbili zilipokutana katika mechi ya hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu, Beki huyo mrefu mwenye asili ya DR Congo aliwavutia mabosi wa Yanga na haraka mabosi wa kikosi hicho wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Hussein Nyika pamoja na aliyekuwa na mjumbe wake, Hamad Islam walinaswa wakifanya maongezi na beki huyo nchini Kigali.
Rwatubyaye amesema, tayari Nyika yuko katika mazungumzo na meneja wake kujadili juu ya uhamisho huo, Hata hivyo, Rwatubyaye ambaye pia ni beki wa kikosi cha kwanza cha timu ya Taifa ya Rwanda 'Amavubi' amesema hata kama Yanga watakubaliana naye bado ana mkataba na Rayon wa mwaka mmoja.
"Yanga ndiyo wameanza mazungumzo rasmi na meneja wangu walinipigia na kutaka mawasiliano naye. Tusubiri kuona kama tutakubaliana na ikiwa hivyo, itabidi pia waongee na Rayon kwa kuwa bado nipo ndani ya mkataba umebaki mwaka mmoja,"alisema Rwatubyaye..
0 comments:
Post a Comment