Saturday, October 27, 2018

Kwa takribani wiki nzima kumekuwa na mjadala unaomuhusu mshambuliaji wa zamani wa Yanga Obrey Chirwa ambaye anataka kurejea Jangwani baada ya kuvunja mkataba na klabu ya Nogotoom inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Misri.

Chirwa ameikacha timu hiyo baada ya kushindwa kumlipa fedha za usajili huku pia ikielezwa Mzambia huyo ameitumikia timu hiyo kwa miezi mitatu bila ya kulipwa mshahara.

Chirwa ndiye aliyeomba kurejea Yanga baada ya kukumbana na changamoto hiyo.
Baada ya ombi hilo viongozi wa Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya usajili Hussein Nyika walimtumia tiketi ya ndege kumleta jijini Dar es salaam kwa ajili ya kumalizana nae.

Hata hivyo matukio aliyofanya Chirwa kabla ya kuondoka Yanga mwishoni mwa msimu uliopita yalimkera kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera ambaye amejitokeza hadharani kupinga usajili wa mshambuliaji huyo 'mtukutu'

Zahera ameonyesha mashaka yake juu ya tabia ya Mzambia huyo ambaye pengine ndiye mchezaji aliyeongoza kwa migomo wakati wote aliokuwa anaitumikia Yanga.

Inaelezwa viongozi wa Yanga tayari wameshamalizana na Chirwa na wamelazimika kufanya jitihada 'kumlainisha' Zahera ili akubali mshambuliaji huyo asajiliwe.

Ukiacha tabia yake, Chirwa ni miongoni mwa washambuliaji wenye vitu vya ziada ambao wanaweza kukupa matokeo wakati wowote.

Inaelezwa Zahera ameridhia mshambuliaji huyo asajiliwe lakini ameutaka uongozi wa Yanga umuwekee masharti ambayo yataepusha matukio yake ya utovu wa nidhamu kuigharimu timu.

Aidha kocha huyo ametaka mshambuliaji huyo amuombe radhi.

Kama usajili wake utafanikiwa, Chirwa atakuwa anarejea Yanga kutengeneza 'pacha' na Heritier Makambo.
Yanga inahitaji kuimarisha safu yake ya ushambuliaji ili kujiongezea nafasi ya kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu.

Washindani wake Simba na Azam Fc safu zao za ushambuliaji zimekamilika wakati Yanga inamtegemea mshambuliaji mmoja tu Heritier Makambo kutokana na kutokuwa na uhakika wa huduma ya Amissi Tambwe ambaye majeruhi ya muda mrefu yamepunguza kasi yakeKwa takribani wiki nzima kumekuwa na mjadala unaomuhusu mshambuliaji wa zamani wa Yanga Obrey Chirwa ambaye anataka kurejea Jangwani baada ya kuvunja mkataba na klabu ya Nogotoom.

0 comments:

Post a Comment