Sunday, November 4, 2018

Beki Andrew Vicent Chikupe amemaliza adhabu ya kufungiwa michezo mitatu na sasa atakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachoikabili Ndanda Fc uwanja wa Taifa keshokutwa.

Chikupe alifungiwa akidaiwa kumpiga kichwa beki wa Simba Mohammed Hussein kwenye mchezo wa watani wa jadi Septemba 30.

Amekosa michezo dhidi ya Alliance, KMC na Lipuli.

Yanga itashuka dimbani Jumapili ikiwa na kikosi chake kamili kwani mbali na Chikupe, wachezaji waliokuwa majeruhi Ibrahim Ajib na Papi Tshishimbi nao wamerejea kikosini

0 comments:

Post a Comment