Mipango ya Manchester United kuwapa mikataba mipya kipa David de Gea, 27, na mshambuliaji Anthony Martial, 22, inatatizwa na mshahara wa pauni 400,000 aliopewa mshambuliaji Alexis Sanchez mwezi January. (Mirror)
Aaron Ramsey huenda akahamia Bayern Munich baada ya mabingwa hao wa Bendesliga kuonyesha nia ya kumsaini mchezaji huyo mweye miaka 27 wakati ataondoka Arsenal msimu ujao. (Express)
Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri anasema viungo wa kati Danny Drinkwater, 28, na Victor Moses, 27, hawako kwenye mipango yake. (Evening Standard)
Chelsea na Manchester City wote wanataka kumsaini mchezaji wa Sunderland mwenye miaka 17, Bali Mumba ambaye amecheza mara nne tu kwenye klabu hiyo ya League One. (Sun)
Tottenham wanataka kumsaini kiungo wa kati wa Colombia Wilmar Barrios kutoka Boca Juniors mwezi Junuary. Mchezaji huyo mwenye miaka 25 anaweza kupatikana kwa puani milioni 16. (Star)
Serikali ya Uingereza itapinga mipango yoyote ya kubuniwa kwa Ligi nyingine ya Ulaya. (Telegraph)
West Ham wanatathmini kumchukua kwa mkopo mshambuliaji wa zamani wa Fulham Kostas Mitroglou mwezi Januari. Mchezaji huyo mwenye miaka 30 kwa sasa yuko Marseille lakini atapatikana. (Daily Mail)
Everton wanataka kumwendea beki wa Crystal Palace Aaron Wan-Bissaka, 20, na wanaweza kumruhusu Ademola Lookman kuhamia upande mwingine kama sehemu ya mkataba. (Sun)
Real Madrid inapania kumnunua kiungo wa kati wa Manchester City Brahim Diaz, 19. (Marca)
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amepinga tetesi kwamba amekuwa akimshawishi mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi, 31, kujiunga na klabu hiyo. (Manchester Evening News)
Mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi, 25, inajiandaa kutia saini mkataba mpya na Inter Milan licha ya vilabu kadhaa vya Ulaya kummezea mate ikiwemo Chelsea. (Calcio Mercato - in Italian)
Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri amesema klabu hiyo haitamsajili mchezaji yeyote wakati wa msimu wa uhamisho wa wachezaji mwezi Januari. (Independent)
Chelsea inataka kutumia fursa ya hali ya switafahamu ya inayokumba Real Madrid kuanzisha mazungumzo ya mkataba mpya na mshambuliaji wa Ubelgiji Eden Hazard.
Kiungo huyo wa miaka 27- huenda akapewa unahodha wa timu endapo atasalia katika ligi ya primia. (Telegraph)
Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino amedokeza azma yake ya kusalia katika klabu hiyo hadi atakapostaafu.(Football.London)
Pochettino amesema haamini kuwa wachezaji nyota wanajitolea kuimarisha klabu hiyo kwa sababu ya uwepo wake. (Sky Sports)
Meneja wa Juventus Massimiliano Allegri hana mpango wa kusajili tena kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 25. (Daily Mirror)
0 comments:
Post a Comment